Add parallel Print Page Options

Walipofika Yerusalemu, mitume, wazee na kanisa lote waliwakaribisha. Paulo, Barnaba, na wengine wakaeleza yote ambayo Mungu alitenda kupitia wao. Baadhi ya waamini mjini Yerusalemu waliokuwa Mafarisayo,[a] walisimama na kusema, “Waamini wasio Wayahudi lazima watahiriwe. Ni lazima tuwaambie waitii Sheria ya Musa!”

Ndipo mitume na wazee wakakusanyika kulichunguza jambo hili.

Read full chapter

Footnotes

  1. 15:5 waamini … Mafarisayo Mtu aliweza kuwa mfuasi wa Yesu na bado akawa Farisayo kama ambavyo baadaye Paulo katika kitabu anasema kuwa yeye ni Farisayo.