Add parallel Print Page Options

Baadhi ya waamini mjini Yerusalemu waliokuwa Mafarisayo,[a] walisimama na kusema, “Waamini wasio Wayahudi lazima watahiriwe. Ni lazima tuwaambie waitii Sheria ya Musa!”

Ndipo mitume na wazee wakakusanyika kulichunguza jambo hili. Baada ya majadiliano ya muda mrefu, Petro akasimama na kuwaambia, “Ndugu zangu, nina uhakika mnakumbuka kilichotokea siku za nyuma. Mungu alinichagua kutoka miongoni mwenu kuzihubiri Habari Njema kwa watu wasio Wayahudi. Kupitia mimi walisikia Habari Njema na kuamini.

Read full chapter

Footnotes

  1. 15:5 waamini … Mafarisayo Mtu aliweza kuwa mfuasi wa Yesu na bado akawa Farisayo kama ambavyo baadaye Paulo katika kitabu anasema kuwa yeye ni Farisayo.