Font Size
Matendo 15:6-8
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Matendo 15:6-8
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
6 Ndipo mitume na wazee wakakusanyika kulichunguza jambo hili. 7 Baada ya majadiliano ya muda mrefu, Petro akasimama na kuwaambia, “Ndugu zangu, nina uhakika mnakumbuka kilichotokea siku za nyuma. Mungu alinichagua kutoka miongoni mwenu kuzihubiri Habari Njema kwa watu wasio Wayahudi. Kupitia mimi walisikia Habari Njema na kuamini. 8 Mungu anamfahamu kila mtu, hata mawazo yao, na amewakubali watu hawa wasio Wayahudi. Amelionyesha hili kwetu kwa kuwapa Roho Mtakatifu kama alivyotupa sisi.
Read full chapter
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International