Add parallel Print Page Options

15 Upepo huu uliichukua meli na kuisukumia mbali. Meli haikuweza kwenda kinyume na upepo, hivyo tulisimama tukijaribu kuuacha upepo utusukume.

16 Tulikwenda upande wa chini wa kisiwa kidogo kilichoitwa Kauda. Kisiwa kikatukinga dhidi ya upepo, tulichukua mtumbwi wa kuokolea watu, lakini ilikuwa vigumu sana kufanya hivyo. 17 Baada ya watu kuleta mtumbwi wa kuokolea, wakaifunga meli kamba kuizungushia ili iendelee kushikamana isipasuke. Waliogopa kwamba meli ingekwama kwenye mchanga wa pwani ya Sirti.[a] Hivyo walishusha tanga na kuiacha meli ichukuliwe na upepo.

Read full chapter

Footnotes

  1. 27:17 pwani ya Sirti Kwa sasa bado ni pwani (Ghuba) ya Sirti katika nchi ya Libya, Afrika ya Kaskazini.