Add parallel Print Page Options

16 Tulikwenda upande wa chini wa kisiwa kidogo kilichoitwa Kauda. Kisiwa kikatukinga dhidi ya upepo, tulichukua mtumbwi wa kuokolea watu, lakini ilikuwa vigumu sana kufanya hivyo. 17 Baada ya watu kuleta mtumbwi wa kuokolea, wakaifunga meli kamba kuizungushia ili iendelee kushikamana isipasuke. Waliogopa kwamba meli ingekwama kwenye mchanga wa pwani ya Sirti.[a] Hivyo walishusha tanga na kuiacha meli ichukuliwe na upepo.

18 Siku iliyofuata upepo ulivuma kinyume nasi kwa nguvu kiasi kwamba watu walitupa baadhi ya vitu kutoka katika shehena ya meli.[b]

Read full chapter

Footnotes

  1. 27:17 pwani ya Sirti Kwa sasa bado ni pwani (Ghuba) ya Sirti katika nchi ya Libya, Afrika ya Kaskazini.
  2. 27:18 walitupa … shehena ya meli Walifanya hivi ili meli iwe nyepesi na isizame kirahisi.