Add parallel Print Page Options

10 Tunataka ninyi nyote na watu wote wa Israeli mtambue kuwa mtu huyu aliponywa na nguvu ya Yesu Kristo kutoka Nazareti. Mlimpigilia Yesu msalabani, lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Mtu huyu alikuwa mlemavu wa miguu, lakini sasa ni mzima. Anaweza kusimama hapa mbele zenu kwa sababu ya nguvu ya Yesu! 11 Yesu ndiye

‘Jiwe[a] ambalo ninyi wajenzi mlilikataa.
    Lakini jiwe hili limekuwa jiwe na msingi.’(A)

12 Yesu peke yake ndiye anayeweza kuokoa watu. Jina lake ndiyo nguvu pekee iliyotolewa kumwokoa mtu yeyote ulimwenguni. Ni lazima tuokoke kupitia yeye!”

Read full chapter

Footnotes

  1. 4:11 Jiwe Alama kumaanisha Yesu.