Add parallel Print Page Options

16 Wakaulizana, “Tuwafanye nini watu hawa? Kila mtu katika Yerusalemu anajua kuhusu muujiza walioufanya kama ishara kutoka kwa Mungu. Ni dhahiri, hatuwezi kusema muujiza huo haukufanyika. 17 Lakini ni lazima tuwatishe ili wasiendelee kuwaambia watu kutumia jina lile.[a] Ili tatizo hili lisisambae miongoni mwa watu.”

18 Hivyo viongozi wa Kiyahudi wakawaita Petro na Yohana ndani tena. Wakawaambia wasiseme wala kufundisha kitu chochote kwa kutumia jina la Yesu.

Read full chapter

Footnotes

  1. 4:17 jina lile Yaani, jina la Yesu. Viongozi wa Kiyahudi walikwepa kutamka jina lake. Tazama Lk 15:2 na Mdo 5:28.