Add parallel Print Page Options

25 Baba yetu Daudi alikuwa mtumishi wako. Kwa msaada wa Roho Mtakatifu aliandika maneno haya:

‘Kwa nini mataifa yanatenda kwa kiburi?
    Kwa nini watu wanapanga mipango isiyofaa kama hii?
26 Wafalme wa dunia hujiandaa kwa mapigano,
    na watawala hukusanyika pamoja kinyume na Bwana
    na kinyume na Masihi wake.’(A)

27 Ndicho hasa kilichotokea wakati Herode, Pontio Pilato, mataifa mengine na watu wa Israeli walipokusanyika pamoja hapa Yerusalemu wakawa kinyume na Yesu; Masihi, Mtumishi wako mtakatifu.

Read full chapter