Paulo na Barnaba walikuwa na mabishano makali nao wakipinga mafundisho haya. Ikaamuliwa kwamba Paulo na Barnaba na waamini wengine waende Yerusalemu wakawaulize mitume na wazee juu ya jambo hili. Kwa hiyo, wakiwa wametumwa na kanisa, njiani walipitia makanisa ya Foenike na Samaria wakatoa taarifa jinsi watu wa mataifa men gine walivyokuwa wakimgeukia Bwana. Habari hizi ziliwafurahisha sana hao ndugu. Walipofika Yerusalemu walipokelewa na kanisa, mitume na wazee; nao wakatoa taarifa kuhusu mambo yote ambayo Mungu aliyafanya kwa kuwatumia wao.

Read full chapter