Kwa hiyo, wakiwa wametumwa na kanisa, njiani walipitia makanisa ya Foenike na Samaria wakatoa taarifa jinsi watu wa mataifa men gine walivyokuwa wakimgeukia Bwana. Habari hizi ziliwafurahisha sana hao ndugu. Walipofika Yerusalemu walipokelewa na kanisa, mitume na wazee; nao wakatoa taarifa kuhusu mambo yote ambayo Mungu aliyafanya kwa kuwatumia wao. Lakini baadhi ya waamini waliokuwa wakishikilia desturi za Mafarisayo wakasema, “Ni lazima watahiriwe na wafundishwe kushika sheria ya Musa.”

Read full chapter