Walipofika Yerusalemu walipokelewa na kanisa, mitume na wazee; nao wakatoa taarifa kuhusu mambo yote ambayo Mungu aliyafanya kwa kuwatumia wao. Lakini baadhi ya waamini waliokuwa wakishikilia desturi za Mafarisayo wakasema, “Ni lazima watahiriwe na wafundishwe kushika sheria ya Musa.”

Mitume na wazee wa kanisa wakakutana kushauriana juu ya jambo hili.

Read full chapter