Lakini baadhi ya waamini waliokuwa wakishikilia desturi za Mafarisayo wakasema, “Ni lazima watahiriwe na wafundishwe kushika sheria ya Musa.”

Mitume na wazee wa kanisa wakakutana kushauriana juu ya jambo hili. Baada ya majadiliano marefu, Petro akasimama na kusema, “Ndugu zangu, mnajua kwamba siku za mwanzo Mungu alini chagua ili kwa midomo yangu watu wa mataifa mengine wapate kusi kia Habari Njema na kuamini.

Read full chapter