Baada ya majadiliano marefu, Petro akasimama na kusema, “Ndugu zangu, mnajua kwamba siku za mwanzo Mungu alini chagua ili kwa midomo yangu watu wa mataifa mengine wapate kusi kia Habari Njema na kuamini. Na Mungu ambaye anajua mioyo ya watu alishuhudia kwamba anawakubali watu wa mataifa kwa kuwapa Roho Mtakatifu kama alivyotupa na sisi. Mungu hakutofautisha kati yetu na wao, bali alitakasa mioyo yao kwa sababu waliamini.

Read full chapter