15 ukaipiga ile meli, na kwa kuwa haikuwa rahisi kushindana nao, tukaiachilia meli isukumwe kuelekea kule upepo unakokwenda. 16 Hatimaye tukasafiri kupitia nyuma ya kisiwa kidogo kiitwacho Kauda, ambapo kwa kuwa tulikuwa tumekingiwa upepo na hicho kisiwa, tuliweza kwa shida kuifunga mashua ya kuokolea watu. 17 Watu walipokwisha ivuta mashua hiyo wakaiingiza katika meli, waliifunga kwa kamba kwenye meli. Kisha, kwa kuogopa kwamba wangesukumwa na upepo mkali na kukwama kwenye mchanga karibu na pwani ya Sirti, walishusha matanga wakaiacha meli ielee.

Read full chapter