17 Watu walipokwisha ivuta mashua hiyo wakaiingiza katika meli, waliifunga kwa kamba kwenye meli. Kisha, kwa kuogopa kwamba wangesukumwa na upepo mkali na kukwama kwenye mchanga karibu na pwani ya Sirti, walishusha matanga wakaiacha meli ielee. 18 Kesho yake dhoruba kali iliendelea kuvuma, kwa hiyo wakaanza kuitupa shehena baharini. 19 Siku ya tatu wakaanza kutupa vifaa vya meli baharini kwa mikono yao wenyewe.

Read full chapter