19 Siku ya tatu wakaanza kutupa vifaa vya meli baharini kwa mikono yao wenyewe. 20 Kwa siku nyingi hatukuona jua wala nyota, na dhoruba kali ilikuwa inaendelea kuvuma. Kwa hiyo tukakata tamaa kabisa kwamba tungeokolewa.

21 Kwa kuwa walikuwa wamekaa siku kadhaa bila kula cho chote, Paulo akasimama kati yao akasema, “Mngenisikiliza wala msingeondoka Krete na kupata mkasa huu na hasara hii.

Read full chapter