Font Size
Matendo Ya Mitume 27:20-22
Neno: Bibilia Takatifu
Matendo Ya Mitume 27:20-22
Neno: Bibilia Takatifu
20 Kwa siku nyingi hatukuona jua wala nyota, na dhoruba kali ilikuwa inaendelea kuvuma. Kwa hiyo tukakata tamaa kabisa kwamba tungeokolewa.
21 Kwa kuwa walikuwa wamekaa siku kadhaa bila kula cho chote, Paulo akasimama kati yao akasema, “Mngenisikiliza wala msingeondoka Krete na kupata mkasa huu na hasara hii. 22 Lakini sasa nawaomba mjipe moyo. Hakuna hata mmoja wenu atakayepoteza maisha yake ila meli hii itaangamia.
Read full chapter
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Copyright © 1989 by Biblica