12 Wokovu unapatikana kwake tu; kwa maana hakuna jina jingine duniani ambalo wamepewa wanadamu kuwaokoa ila jina la Yesu, na ni kwa jina hilo peke yake tunaweza kuokolewa!”

Ujasiri Wa Petro Na Yohana Washangaza Watu

13 Wale viongozi na wazee walipoona ujasiri wa Petro na Yohana na kufahamu ya kuwa walikuwa watu wa kawaida wasio na elimu walishangaa sana. Wakatambua kwamba hawa watu walikuwa na Yesu. 14 Lakini kwa kuwa walimwona yule kilema aliyeponywa ame simama nao hawakuweza kusema lo lote kupinga maneno yao.

Read full chapter