16 Kisha wakaanza kuulizana, “Tuwafanye nini watu hawa? Hatuwezi kukanusha muujiza huu mkubwa walioufanya ambao ni dhahiri kwa kila mtu Yerusalemu. 17 Lakini tunaweza kuzuia jambo hili lisiendelee kuenezwa kwa watu kama tukiwakanya wasiseme tena na mtu ye yote kwa jina la Yesu.” 18 Kwa hiyo wakawaita tena ndani wakawaamuru wasiseme au kufundisha watu tena kwa jina la Yesu.

Read full chapter