Add parallel Print Page Options

16 Yakobo alikuwa baba yake Yusufu,

Yusufu alikuwa mume wa Mariamu.

Na Mariamu alimzaa Yesu, anayeitwa Masihi.

17 Kulikuwa na vizazi kumi na nne kuanzia kwa Ibrahimu mpaka kwa Daudi. Na kulikuwa na vizazi kumi na nne kuanzia kwa Daudi mpaka wakati wa uhamisho wa Babeli. Na palikuwa na vizazi kumi na nne tangu uhamisho wa Babeli mpaka wakati alipozaliwa Yesu, Masihi.

Kuzaliwa kwa Yesu, Masihi

(Lk 2:1-7)

18 Kuzaliwa kwa Yesu Masihi, kulikuwa hivi: Mariamu mama yake alikuwa amechumbiwa na Yusufu. Kabla hawajaoana, Yusufu aligundua kuwa Mariamu alikuwa mja mzito. (Yeye alipata mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.)

Read full chapter