Font Size
Mathayo 10:14-16
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Mathayo 10:14-16
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
14 Na ikiwa watu katika nyumba au mji watakataa kuwapokea au kuwasikiliza, basi ondokeni mahali hapo na mkung'ute mavumbi kutoka katika miguu yenu. 15 Ninaweza kuwathibitishia kuwa siku ya hukumu itakuwa vibaya sana kwa mji huo kuliko watu wa Sodoma na Gomora.[a]
Yesu Aonya Kuhusu Matatizo
(Mk 13:9-13; Lk 21:12-17)
16 Sikilizeni! Ninawatuma, nanyi mtakuwa kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. Hivyo muwe na akili kama nyoka. Lakini pia muwe kama njiwa na msimdhuru yeyote.
Read full chapterFootnotes
- 10:15 Sodoma na Gomora Miji ambayo Mungu aliiangamiza kwa sababu watu waliokuwa wakiishi pale walikuwa waovu sana. Tazama Mwa 19.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International