Add parallel Print Page Options

17 Ikiwa mtu aliyetenda dhambi atakataa kuwasikiliza, ndipo uliambie kanisa. Na akikataa kulisikiliza kanisa, mchukulie kama ambavyo ungemchukulia mtu asiyemfahamu Mungu au mtoza ushuru.

18 Ninawahakikishia kuwa mnapotoa hukumu hapa duniani, hukumu hiyo itakuwa hukumu ya Mungu. Na mnapotoa msamaha, nao utakuwa msamaha wa Mungu.[a] 19 Kwa namna nyingine, ikiwa watu wawili waliopo duniani watakubaliana kwa kila wanachokiombea, Baba yangu wa mbinguni atatenda kile wanachokiomba.

Read full chapter

Footnotes

  1. 18:18 mnapotoa msamaha … wa Mungu Kwa maana ya kawaida, “chochote mtakachokifunga hapa duniani kitakuwa kimefungwa mbinguni, na chochote mtakachokifungua kitakuwa kimefunguliwa mbinguni”.