Font Size
Mathayo 19:11-13
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Mathayo 19:11-13
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
11 Akajibu, “Tamko hili ni la kweli kwa baadhi ya watu, lakini si kwa kila mtu. Bali ni kwa wale tu waliopewa karama hii. 12 Kuna sababu tofauti kwa nini baadhi ya wanaume hawaoi.[a] Wengine wamezaliwa wakiwa hawana uwezo wa kuzaa watoto, wengine walifanywa hivyo katika maisha yao ya baadaye. Na wengine walichagua kutokuoa kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Hili liko hivyo kwa kila anayeweza kulikubali.”
Yesu Awakaribisha Watoto
(Mk 10:13-16; Lk 18:15-17)
13 Ndipo watu wakawaleta watoto wao wadogo kwa Yesu ili awabariki na kuwaombea. Wafuasi wake walipoliona hili, waliwakataza watu wasiwalete watoto kwa Yesu.
Read full chapterFootnotes
- 19:12 wanaume hawaoi Kwa maana ya kawaida, “Maana wapo walio matowashi”.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International