Add parallel Print Page Options

12 Kuna sababu tofauti kwa nini baadhi ya wanaume hawaoi.[a] Wengine wamezaliwa wakiwa hawana uwezo wa kuzaa watoto, wengine walifanywa hivyo katika maisha yao ya baadaye. Na wengine walichagua kutokuoa kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Hili liko hivyo kwa kila anayeweza kulikubali.”

Yesu Awakaribisha Watoto

(Mk 10:13-16; Lk 18:15-17)

13 Ndipo watu wakawaleta watoto wao wadogo kwa Yesu ili awabariki na kuwaombea. Wafuasi wake walipoliona hili, waliwakataza watu wasiwalete watoto kwa Yesu. 14 Lakini Yesu akasema, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie, kwa sababu ufalme wa Mungu ni wa watu walio kama watoto hawa wadogo.”

Read full chapter

Footnotes

  1. 19:12 wanaume hawaoi Kwa maana ya kawaida, “Maana wapo walio matowashi”.