Add parallel Print Page Options

55 Kisha Yesu akaliambia kundi, “Kwa nini mnakuja kunikamata mkiwa na mikuki na marungu kama vile mimi ni mhalifu? Nimekuwa nakaa eneo la Hekalu nikifundisha kila siku. Kwa nini hamkunikamata kule? 56 Lakini mambo haya yote yametokea ili kutimiza Maandiko yaliyoandikwa na manabii.” Ndipo wafuasi wake wote wakamwacha na kukimbia.

Yesu Akiwa Mbele ya Viongozi wa Kidini

(Mk 14:53-65; Lk 22:54-55,63-71; Yh 18:13-14,19-24)

57 Wale waliomkamata Yesu wakampeleka nyumbani kwa Kayafa, kuhani mkuu. Walimu wa Sheria na viongozi wazee wa Kiyahudi walikuwa wamekusanyika huko.

Read full chapter