Add parallel Print Page Options

Yohana alisema, “Tubuni na kuibadili mioyo yenu, kwa sababu ufalme wa Mungu umekaribia.” Nabii Isaya alisema kuhusu habari za Yohana Mbatizaji pale aliposema,

“Kuna mtu anayeipaza sauti yake toka nyikani:
‘Tayarisheni njia kwa ajili ya Bwana;
    nyoosheni njia kwa ajili yake.’”(A)

Huyo Yohana alivaa mavazi yaliyofumwa kutokana na manyoya ya ngamia. Naye alijifunga mkanda wa ngozi kuzunguka kiuno chake, na alikula nzige na asali mbichi.

Read full chapter