Add parallel Print Page Options

16 Watu wanaoishi katika giza ya kiroho,
    nao wameiona nuru iliyo kuu.
Nuru hiyo imeangaza kwa ajili yao wale
    wanaoishi katika nchi yenye giza kama kaburi.”(A)

17 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaambia watu ujumbe wake unaosema, “Mbadili mioyo yenu na maisha yenu pia, kwa sababu Ufalme wa Mungu umewafikia.”

Yesu Achagua Baadhi ya Wafuasi

(Mk 1:16-20; Lk 5:1-11)

18 Yesu alipokuwa akitembea kando ya Ziwa Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni, aitwaye Petro na nduguye aitwaye Andrea. Ndugu hawa walikuwa wavuvi na walikuwa wanavua samaki kwa nyavu zao.

Read full chapter