Add parallel Print Page Options

16 Kwa namna hiyo hiyo mnapaswa kuwa nuru kwa ajili ya watu wengine. Hivyo ishini katika namna ambayo watakapoyaona matendo yenu mema, watamtukuza Baba yenu wa mbinguni.

Yesu Afundisha Kuhusu Sheria ya Musa

17 Msifikiri kwamba nimekuja kuiharibu Sheria ya Musa au mafundisho ya manabii. Sikuja kuyaharibu mafundisho yao bali kuyakamilisha. 18 Ninawahakikishia kuwa hakuna jambo litakaloondolewa katika sheria mpaka mbingu na nchi zitakapopita. Hakuna hata herufi ndogo ama nukta katika Sheria ya Musa itakayotoweka mpaka hapo itakapotimizwa.

Read full chapter