Font Size
Mathayo 5:20-22
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Mathayo 5:20-22
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
20 Ninawambia, ni lazima muitii sheria ya Mungu kwa kiwango bora kuliko kile cha walimu wa sheria na Mafarisayo. La sivyo, hamtaweza kuingia katika ufalme wa Mungu.
Yesu Afundisha Kuhusu Hasira
21 Mmesikia kuwa hapo kale baba zetu waliambiwa, ‘Usimwue yeyote. Na yeyote atakayeua atahukumiwa.’(A) 22 Lakini ninawaambia, msimkasirikie mtu yeyote kwa sababu mkifanya hivyo mtahukumiwa. Na mkimtukana mtu yeyote, vivyo hivyo mtahukumiwa na baraza kuu. Na ukimwita mtu kuwa ni mjinga, utakuwa katika hatari ya kutupwa kwenye moto wa Jehanamu.
Read full chapter
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International