Font Size
Mathayo 8:1-3
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Mathayo 8:1-3
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Yesu Amponya Mgonjwa
(Mk 1:40-45; Lk 5:12-16)
8 Yesu alipotelemka kutoka kwenye kilima, umati mkubwa wa watu ulimfuata. 2 Mtu mmoja mwenye ugonjwa mbaya sana wa ngozi akamwendea, akainama mbele yake mpaka chini na akasema, “Bwana ukitaka una uwezo wa kuniponya.”
3 Yesu aliunyoosha mkono wake akamshika mtu yule mwenye ugonjwa mbaya sana wa ngozi. Akasema, “Hakika, ninataka kukuponya. Upone!” Mtu huyo akapona ugonjwa mbaya sana wa ngozi saa hiyo hiyo.
Read full chapter
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International