Add parallel Print Page Options

Kisha Yesu akamwambia, “Usimwambie mtu yeyote kilichotokea, lakini nenda kwa kuhani akakuchunguze.[a] Na umtolee Mungu sadaka ambazo Musa aliamuru watu wanaoponywa watoe, ili iwe ushahidi kwa watu kwamba umepona.”

Yesu Amponya Mtumishi wa Afisa wa Jeshi

(Lk 7:1-10; Yh 4:43-54)

Yesu alikwenda Kapernaumu. Alipoingia mjini, afisa wa jeshi alimjia na kumwomba msaada. Akasema, “Bwana, mtumishi wangu ni mgonjwa sana nyumbani na amelala kitandani. Hawezi hata kutingishika na ana maumivu makali sana.”

Read full chapter

Footnotes

  1. 8:4 kuhani akakuchunguze Sheria ya Musa (torati) ilisema kuhani ni lazima aamue ikiwa mtu amepona ukoma.