14 Watasema, ‘Yale matunda ambayo roho yako iliy atamani yametoweka, na utajiri wako wote na ufahari vimetoweka, wala hutavipata kamwe!’

15 Wale wafanya biashara wa bidhaa hizo waliopata utajiri wao kwake watasimama mbali kabisa kwa kuogopa mateso yake, nao watalia na kuomboleza kwa nguvu wakisema, 16 ‘Ole wako! Ole wako! mji mkuu, ulikuwa umevikwa mavazi ya kitani safi, rangi ya zambarau na nyekundu, uking’aa kwa dhahabu na vito vya thamani na lulu!

Read full chapter