16 ‘Ole wako! Ole wako! mji mkuu, ulikuwa umevikwa mavazi ya kitani safi, rangi ya zambarau na nyekundu, uking’aa kwa dhahabu na vito vya thamani na lulu! 17 Katika muda wa saa moja utajiri wote huu umeharibiwa!’ Manahodha wote, mabaharia na wote wasafirio baharini na wote wafanyao kazi melini watasimama mbali kabisa.

18 Watakapoona moshi wake wakati mji ukiteketezwa watalia wakisema, ‘Kuna mji gani ambao umepata kuwa kama mji huu mkuu?’

Read full chapter