17 Katika muda wa saa moja utajiri wote huu umeharibiwa!’ Manahodha wote, mabaharia na wote wasafirio baharini na wote wafanyao kazi melini watasimama mbali kabisa.

18 Watakapoona moshi wake wakati mji ukiteketezwa watalia wakisema, ‘Kuna mji gani ambao umepata kuwa kama mji huu mkuu?’ 19 Nao watajimwagia vumbi vichwani na kulia na kuomboleza wakisema, ‘Ole wako, Ole wako mji mkuu, mji ambapo wote wenye meli baharini walitajirika kwa mali yake! Maana katika saa moja tu umeteketezwa.

Read full chapter