20 Fura hini juu yake, enyi mbingu, watakatifu na mitume na manabii; Kwa kuwa Mungu ameuhukumu kwa ajili yenu!”’

21 Kisha malaika mkuu akachukua jiwe kama jiwe kubwa la kusagia akalitupa baharini akisema, ‘ ‘Hivyo ndivyo mji mkuu wa Babiloni utakavyotupwa chini kwa nguvu wala hautaonekana kamwe. 22 Wala sauti za wapiga vinanda, na wapiga zomari, wapiga fil imbi na sauti ya wapiga tarumbeta hazitasikika kwako kamwe. Hata patikana kwako fundi mwenye ujuzi wo wote; wala sauti ya jiwe la kusaga haitasikika kamwe.

Read full chapter