21 Kisha malaika mkuu akachukua jiwe kama jiwe kubwa la kusagia akalitupa baharini akisema, ‘ ‘Hivyo ndivyo mji mkuu wa Babiloni utakavyotupwa chini kwa nguvu wala hautaonekana kamwe. 22 Wala sauti za wapiga vinanda, na wapiga zomari, wapiga fil imbi na sauti ya wapiga tarumbeta hazitasikika kwako kamwe. Hata patikana kwako fundi mwenye ujuzi wo wote; wala sauti ya jiwe la kusaga haitasikika kamwe. 23 Na nuru ya taa haitaangaza ndani yako tena; Wala sauti ya bwana harusi na bibi harusi haitasikiwa ndani yako kamwe. Maana wafanya biashara wako walikuwa watu maarufu wa duniani, na mataifa yote yalidanganyika kwa uchawi wako.

Read full chapter