Font Size
Ufunua wa Yohana 18:22-24
Neno: Bibilia Takatifu
Ufunua wa Yohana 18:22-24
Neno: Bibilia Takatifu
22 Wala sauti za wapiga vinanda, na wapiga zomari, wapiga fil imbi na sauti ya wapiga tarumbeta hazitasikika kwako kamwe. Hata patikana kwako fundi mwenye ujuzi wo wote; wala sauti ya jiwe la kusaga haitasikika kamwe. 23 Na nuru ya taa haitaangaza ndani yako tena; Wala sauti ya bwana harusi na bibi harusi haitasikiwa ndani yako kamwe. Maana wafanya biashara wako walikuwa watu maarufu wa duniani, na mataifa yote yalidanganyika kwa uchawi wako. 24 Na ndani yake ilikutwa damu ya manabii na watakatifu na watu wote waliouawa duniani.”
Read full chapter
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Copyright © 1989 by Biblica