Aliyepanda Farasi Mweupe

11 Kisha nikaona mbingu imefunguka na mbele yangu nikaona farasi mweupe! Aliyeketi juu ya huyo farasi aliitwa Mwaminifu na Kweli, naye huhukumu na kupigana vita kwa ajili ya haki. 12 Macho yake ni kama miali ya moto na juu ya kichwa chake kuna vilemba vingi; na ameandikwa jina ambalo hakuna mwingine anayeli jua isipokuwa yeye mwenyewe. 13 Amevaa vazi lililochovywa katika damu na jina analoitwa ni “Neno la Mungu”.

Read full chapter