15 Kinywani mwake mlitoka upanga mkali wa kuyapiga mataifa. Atawatawala kwa fimbo ya chuma na kukamua divai katika mtambo wa kutengenezea divai ya ghadhabu ya Mungu Mwenyezi. 16 Kwenye vazi lake na paja lake liliandikwa jina hili: “Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.”

Bwana wa mabwana.”

17 Kisha nikamwona malaika amesimama ndani ya jua, akaita ndege wote warukao angani kwa sauti kuu, “Njooni, kusanyikeni kwa ajili ya karamu kubwa ya Mungu.

Read full chapter