Alipewa kitani safi nyeupe inayong’aa ili avae.” Hiyo kitani safi ni matendo ya haki ya watakatifu.

Na malaika akaniambia, “Andika haya: ‘Wamebarikiwa wal ioalikwa kwenye karamu ya harusi ya Mwana-Kondoo.”’ Na akaniambia, “Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.”

10 Ndipo nikaanguka kifudifudi miguuni pake kumwabudu, lakini yeye akaniambia, “Usifanye hivyo! Mimi pia ni mtumishi pamoja na wewe na ndugu zako wanaoshikilia ushuhuda wao kwa Yesu. Mwabudu Mungu! Maana ushuhuda wa Yesu ndio kiini cha unabii.”

Read full chapter