Na malaika akaniambia, “Andika haya: ‘Wamebarikiwa wal ioalikwa kwenye karamu ya harusi ya Mwana-Kondoo.”’ Na akaniambia, “Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.”

10 Ndipo nikaanguka kifudifudi miguuni pake kumwabudu, lakini yeye akaniambia, “Usifanye hivyo! Mimi pia ni mtumishi pamoja na wewe na ndugu zako wanaoshikilia ushuhuda wao kwa Yesu. Mwabudu Mungu! Maana ushuhuda wa Yesu ndio kiini cha unabii.”

Aliyepanda Farasi Mweupe

11 Kisha nikaona mbingu imefunguka na mbele yangu nikaona farasi mweupe! Aliyeketi juu ya huyo farasi aliitwa Mwaminifu na Kweli, naye huhukumu na kupigana vita kwa ajili ya haki.

Read full chapter