10 Na yule Ibilisi aliyewadanganya alitupwa katika ziwa la moto na kiberiti walipokuwa yule mnyama na yule nabii wa uwongo. Nao watateseka huko usiku na mchana, milele na milele.

11 Kisha nikaona kiti kikubwa cha enzi cheupe, pamoja na huyo aliyeketi juu yake. Dunia na anga zilikimbia kutoka machoni pake zikatoweka wala hazikuonekana tena. 12 Nikaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya kiti cha enzi, na vitabu vikafunguliwa. Pia kitabu kingine ambacho ni kitabu cha uzima kikafunguliwa. Na hao wafu wakahukumiwa kutokana na yale yaliy oandikwa ndani ya vitabu hivyo, kuhusu matendo yao.

Read full chapter