Nao walitembea juu ya eneo lote la dunia, wakaizunguka kambi ya wata katifu na ule mji mwema, lakini moto ulishuka kutoka mbinguni, ukawateketeza. 10 Na yule Ibilisi aliyewadanganya alitupwa katika ziwa la moto na kiberiti walipokuwa yule mnyama na yule nabii wa uwongo. Nao watateseka huko usiku na mchana, milele na milele.

11 Kisha nikaona kiti kikubwa cha enzi cheupe, pamoja na huyo aliyeketi juu yake. Dunia na anga zilikimbia kutoka machoni pake zikatoweka wala hazikuonekana tena.

Read full chapter