Yerusalemu Mpya

21 Kisha nikaona mbingu mpya na dunia mpya; maana mbingu ya kwanza na dunia ya kwanza zilikwisha kutoweka na bahari haikuwapo tena. Ndipo nikaona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, ukiwa umeandaliwa kama bibi harusi aliyepambwa kwa bwana wake.

Read full chapter