Yerusalemu Mpya

21 Kisha nikaona mbingu mpya na dunia mpya; maana mbingu ya kwanza na dunia ya kwanza zilikwisha kutoweka na bahari haikuwapo tena. Ndipo nikaona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, ukiwa umeandaliwa kama bibi harusi aliyepambwa kwa bwana wake. Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, “Tazama, maskani ya Mungu yako pamoja na wanadamu, naye ataishi pamoja nao. Watakuwa watu wake, na Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, naye atakuwa Mungu wao.

Read full chapter