Atafuta machozi yao yote, na kifo hakitakuwepo tena, wala maom bolezo, wala kilio, wala maumivu; maana mambo hayo yote ya awali yamekwisha toweka.”

Na yule aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi akasema, “Tazama, nafanya kila kitu kuwa kipya.” Pia akasema, “Andika haya, maana maneno haya ni ya kuaminika, tena ni ya kweli.” Akaniambia, “Yamekamilika! Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho. Walio na kiu nitawapa maji kutoka katika chemchemi ya maji ya uzima bila malipo.

Read full chapter