Akaniambia, “Yamekamilika! Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho. Walio na kiu nitawapa maji kutoka katika chemchemi ya maji ya uzima bila malipo. Atakayeshinda atarithi baraka zote hizi, na mimi nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. Lakini waoga, na wasioamini na wachafu, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na wanaoabudu sanamu, pamoja na waongo wote, urithi wao upo katika lile ziwa linalowaka moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili.”

Read full chapter