Atakayeshinda atarithi baraka zote hizi, na mimi nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. Lakini waoga, na wasioamini na wachafu, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na wanaoabudu sanamu, pamoja na waongo wote, urithi wao upo katika lile ziwa linalowaka moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili.”

Kisha mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na mabakuli saba ya yale maafa saba ya mwisho akaja akaniambia, “Njoo, nitakuon yesha bibi harusi, mke wa Mwana-Kondoo.”

Read full chapter