Lakini waoga, na wasioamini na wachafu, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na wanaoabudu sanamu, pamoja na waongo wote, urithi wao upo katika lile ziwa linalowaka moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili.”

Kisha mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na mabakuli saba ya yale maafa saba ya mwisho akaja akaniambia, “Njoo, nitakuon yesha bibi harusi, mke wa Mwana-Kondoo.”

10 Basi, nikiwa katika Roho, akanipeleka mbali kwenye mlima mkubwa na mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu.

Read full chapter