Kisha mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na mabakuli saba ya yale maafa saba ya mwisho akaja akaniambia, “Njoo, nitakuon yesha bibi harusi, mke wa Mwana-Kondoo.”

10 Basi, nikiwa katika Roho, akanipeleka mbali kwenye mlima mkubwa na mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu. 11 Ulikuwa na utukufu wa Mungu, uking’aa kama kito cha thamani sana, kama yaspa, na safi kama kioo.

Read full chapter